Mpanda FM
Mpanda FM
19 May 2025, 2:50 pm

‘Waishi kwa kufuata maelekezo na misingi ya imani mwenyezi Mungu.‘
Na Samwel Mbugi -Katavi
Sheikh mkuu wa mkoa wa Katavi Nassor Kakulukulu amewataka waumini wa dini ya Kiislam mkoani Hapa kuachana na uovu na badala yake waishi kwa kufuata maelekezo na misingi ya imani mwenyezi Mungu.
Shekh Kakulukulu amesema kuwa baadhi ya waumini wamekuwa hawana msimamo wa kiimani wanaheshimu mwezi mtukufu pekee.
Kwa upande wao baadhi ya waumini wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuwaomba viongozi wao kwenda kutoa elimu ya kimaadili katika makundi ya vijana.