Mpanda FM
Mpanda FM
19 May 2025, 2:18 pm

‘miradi mingi imetekelezwa na kukamilika na inaleta manufaa kwa wananchi wa halmashauri hiyo.’
Na Betord Chove -Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kwa utekelezaji mahili wa miradi ya kimikakati inayoendelea wilayani hapo kutokana na mapato ya ndani ya biashara ya kaboni.
Akizungumza katika Baraza maalumu la madiwani lililoketi kwa ajili ya kujadili taarifa za utekelezaji wa miradi ya Bakaa inayoendelea na miradi ya kimikakati katika halmashauri ya wilaya Tanganyika amesema miradi mingi imetekelezwa na kukamilika na inaleta manufaa kwa wananchi wa halmashauri hiyo.
Akitoa taarifa ya hali halisi ya uwekezaji wa miradi ya kimkakati afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Deus Luziga amesema vijiji kupitia mapato yake ya awamu ya Tisa na Kumi vilitenga jumla ya Shs. 436,000,000.
Kwa upande wake afisa tawala msaidizi uchumi na uzalishaji Nehemia James akizungumza na madiwani wa Halmashauri hiyo amewashauri kuwekeza katika miradi ambayo itatua changamoto za wananchi kama vile changamoto za ufugaji Kwa kuanzisha ufugaji wa kisasa ili kupunguza idadi ya mifugo