Mpanda FM
Mpanda FM
3 May 2025, 11:59 am

Picha ya waombolezaji. Picha na Samwel Mbugi
“Tunaonewa sisi wanyonge”
Na Beny Gadau
Wananchi wa mtaa wa Ilembo manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameitaka serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wa kifo cha Ediga Mwaniwe mfanyabiashara na mchimbaji wa madini eneo la magula Mkoani Katavi.
Wakizungumza na Mpanda redio fm baadhi ya wananchi wamesema kuwa kijana huyo alishambuliwa na baadhi ya watu akihisiwa kuuza dhahabu feki katika moja ya kampuni ya ununuaji wa dhahabu iliyopo kitongoji cha Magula.
Kaka wa marehemu Charles Mwaniwe ameliomba jeshi la polisi Mkoani hapa kutenda haki kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria dhidi ya wote waliohusika na tukio la kumshambulia mdogo wake hadi kupoteza maisha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi Mkoani Katavi April 28 imesema kuwa wanawashikiria watu saba ambao ni Fredrick AZIZ (24) Langula Mbiha (36) Kurwa Alphonce (36) Kashindye Saidi (32) Molah John (35) Joseph Japhet (30) na John Shuli (30) Kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Edga Mwaniwe. Aidha jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wawasilishe changamoto zao kwa mamlaka husika kwa ajili ya ufumbuzi.