Mpanda FM

Maadhimisho ya zimamoto wananchi watoa neno

3 May 2025, 11:40 am

Picha ya afisa habari msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Katavi. Picha na Anna Mhina.

“Lengo la maadhimisho ni kuwakumbuka waliopoteza maisha wakiwa kazini”

Na Anna Mhina

Baadhi ya wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuimarisha vitendea kazi katika jeshi la zimamoto na uokoaji.

Wito huo umekuja kufuatia maadhimisho ya wiki ya zimamoto duniani ndipo wananchi hao walipofunguka na kukiri kuwa wanatambua umuhimu wa jeshi la zimamoto na uokoaji na kuiomba serikali iboreshe miundo mbinu.

Sauti ya wananchi

Kwa upande wake Afisa habari wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa Catherine Sambagi ameeleza lengo la kuanzisha maadhimisho hayo ikiwemo kutoa heshima na kumbukumbu kwa zimamoto waliopoteza maisha wakiwa kazini.

Sauti ya afisa habari

Maadhimisho haya yameanza rasmi may 4 mwaka 1999 kufuatia tukio la kusikitisha lililotokea nchini Australia ambapo zimamoto watano walipoteza maisha wakijaribu kuzima moto mkubwa wa msitu katika jimbo la Victoria.