Mpanda FM
Mpanda FM
16 April 2025, 1:44 pm

Picha ya mkuu wa wilaya ya Mpanda. Picha na Anna Mhina
“Wananchi mchukue tahadhari kipindi hiki cha mvua”
Na Anna Mhina
Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha baadhi ya mawasiliano ya barabara kukatika Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari katika kuwalinda Watoto.
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph kufuatia kipindi hiki cha likizo kwa wanafunzi na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameeleza namna ambavyo watawalinda watoto wao kipindi hiki cha likizo ili kuweza kuwaepusha na majanga mbalimbali.