Mpanda FM

Hofu yatanda kwa wananchi wa Kasimba, chatu mwingine auwawa

27 March 2025, 3:36 pm

Picha ya chatu aliyeuawa. Picha na Anna Mhina

“Naomba nitoe rai sitisheni shughuli zote katika mto huo”

Na Anna Mhina

Wananchi wa mtaa wa Kasimba uliopo kata ya Ilembo wilayani Mpanda mkoani Katavi  wameingiwa hofu baada ya kuuawa kwa nyoka aina ya chatu.

Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wameeleza kuwa wamegundua uwepo wa chatu huyo baada ya kuingia kwenye moja ya nyumba ya mkazi wa eneo hilo.

Sauti za wananchi

Nae mwenyekiti wa mtaa wa Kasimba Benard Nswima ametoa rai kwa wananchi kusitisha shughuli zote katika mto huo.

Sauti ya mwenyekiti

Ikumbukwe kuwa january 15 mwaka huu aliuawa chatu mwenye urefu wa futi 12 akiwa amemeza mbuzi na february 4 alionekana chatu mwingine akiwa amemeza mbwa katika mtaa wa Msasani jirani na mtaa wa Kasimba.