

16 March 2025, 3:25 pm
“Wananchi wanachelewa kutoa taarifa kwa jeshi la zimamoto na uokoaji”
Na Anna Mhina
Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameliomba jeshi la zimamoto na uokoaji kuweka mifumo bora ili kuweza kufika kwa wakati pindi wanapopokea taarifa za dharura.
Wakizungumza na Mpanda Radio FM wananchi hao wamelilalamikia jeshi la zimamoto na uokoaji kutofika kwa wakati eneo la tukio na kuiomba serikali iboreshe miundombinu ya vitendea kazi katika jeshi hilo.
Akijibu malalamiko hayo afisa habari wa jeshi hilo mkoa wa Katavi Catherine Sambagi amesema kuwa wananchi wanachelewa kutoa taarifa hali inayowasababisha kushindwa kufika eneo la tukio kwa wakati.
Mojawapo wa njia inayotumiwa kutoa taarifa ya dharura kwa jeshi la zimamoto na uokoaji inapotokea ni kupiga namba 114.