

11 March 2025, 3:39 pm
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akizungumza na wananchi msibani. Picha na Anna Mhina
“Wananchi mchukue tahadhari mnapoenda porini”
Na Anna Mhina
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Adeniza Spriano mwenye umri wa miaka 63 mkazi wa kijiji cha Mtambo kilichopo kata ya Katumba walayani Mpanda mkoani Katavi amefariki dunia baada ya kukanyagwa na tembo.
Akizungumza na Mpanda radio FM mwenyekiti wa kitongoji cha Majengo kilichopo katika kijiji hicho Dickson Obadia ameeleza kuwa tukio hilo limetoka machi 9, 2025 baada ya marehemu kwenda shambani kuokota kuni ndipo alipovamiwa na tembo hadi kupelekea umauti.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapoamefika nyumbani kwa marehemu na ajili ya kutoa mkono wa pole na kuwataka wananchi kuchukua tahadhali katika eneo hilo.