

11 March 2025, 2:36 pm
Picha ya madarasa yaliyoezuliwa. Picha na Anna Mhina
“Hakikisha miundombinu ya madarasa inajengwa kwa wakati”
Na Anna Mhina
Shule ya msingi Ivungwe iliyopo kata ya Katumba halmashauri ya Nsimbo wilayani Mpanda mkoani Katavi imeezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha march 8, mwaka huu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwalimu mkuu wa shule hiyo Maiko Cosmas ameeleza namna tukio lilivyotokea na hatua walizozichukua.
Kwa upande wake Injinia Salimu Kisaka ameeleza kuwa gharama za madarasa mapya yanayotakiwa kujengwa yakiwa na viwango vinavyotakiwa yatagharimu zaidi ya million 70.
Mkuu wa wilaya ya Mpanda amefika shuleni hapo na kujionea uharibifu uliojitokeza ambapo ametoa maelekezo kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha miundombinu ya madarasa inajengwa kwa wakati ili kusaidia wanafunzi kuendelea na masomo.