Mpanda FM

Madereva watakiwa kuacha matumizi ya simu wanapokuwa barabarani

25 February 2025, 4:20 pm

Picha ya wasafirishaji wa vyombo vya moto. Picha na Anna Mhina

“Hatua zitachukuliwa kwa dereva atakaebainika amevunja sheria”

Na Edda Enock

Madereva wa vyombo vya moto mkoani Katavi wametakiwa kuacha matumizi ya simu wakiwa barabarani ili kuepukana na ajali zinazoepukika.

Wito huo umetolewa na mkaguzi msaidizi wa polisi Geofrey Brithon wakati akizungumza na Mpanda radio FM  ambapo amesema kuwa sheria zitachukuliwa kwa mtu atakaebainika kutumia simu huku akiwa anaendesha chombo cha moto.

Sauti ya mkaguzi wa polisi

Nao baadhi ya madereva wameonekana kutokuelewa athari zinazoweza kujitokeza pindi wanapotumia simu wakiwa barabarani.

Sauti ya madereva

Utafiti unaonyesha kuwa madereva wanaotumia simu wana uwezekano mkubwa wa kufanya makosa, kama vile kupita alama za kusimama au kuingilia kwenye njia za madereva wengine.