

20 February 2025, 10:32 am
Picha ya F9052 PC John Shindika. Picha na Anna Mhina
“Tunahitaji elimu itolewe kwenye vijiwe vya bodaboda”
Na Anna Mhina
Kutokana na baadhi ya madereva wa vyombo vya moto kutotii sheria za usalama barabarani hususani mataa Jeshi la polisi mkoani Katavi kitengo cha usalama barabarani limewataka madereva hao kuacha tabia hiyo ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
Akizungumza na Mpanda radio media F9052 PC John Shindika kutoka ofisi ya mkuu wa usalama barabarani mkoa amesema wamejipanga kuwachukulia hatua madereva watakaobainika wanavunja sheria ikiwemo faini na kupelekwa mahakamani.
Kwa upande wao baadhi ya madereva wameeleza kuwa uvunjifu wa sheria unasababishwa na ukosefu wa elimu ya matumizi sahihi ya taa huku wengine wakiwa na mtazamo tofauti.