

18 February 2025, 2:19 pm
Picha ya mmoja kati ya wadau waliopatiwa vyeti na Kamanda Ngonyani. Picha na Anna Mhina
“Askari polisi na wadau waliofanya kazi vizuri wapatiwa vyeti”
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limetoa vyeti kwa askari polisi waliofanya kazi vizuri na wadau mbalimbali wanaoonesha ushirikiano kulisaidia jeshi kulinda usalama wa raia na mali zao.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kastar Ngonyani amesema amefanya zoezi hilo la kuwapa zawadi baadhi ya askari waliofanya vizuri pamoja na kutoa vyeti kwa baadhi ya wadau kwa niaba ya mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Camillus Wambura.
Kwa upande wao baadhi ya wadau waliopata vyeti wametoa shukrani kwa jeshi la polisi mkoa wa Katavi kwa kutambua mchango wao katika kulinda amani ya mkoa na Taifa kwa ujumla.
Ngonyani amesema jumla ya askari polisi waliopatiwa vyeti pamoja na wadau mbalimbali ni 29.