

7 February 2025, 2:29 pm
Picha ya Koplo Zainabu Yusuph. Picha na Samwel Mbugi
“Ukatili kwa watoto wa kambo huathiri afya ya akili ya mtoto”
Na Lilian Vicent
Baadhi ya wananchi mkoa wa Katavi wamesema kuwa familia nyingi kuvunjika miongoni mwa wazazi ni moja ya sababu inayopelekea kuongezeka kwa watoto wakufikia au wakambo ambao wamekuwa wakinyanyasika katika malezi.
Wakizungumza na Mpanda redio FM wamebainisha kuwa wazazi wanapaswa kuwa karibu na watoto ili kubaini matukio hayo.
Koplo Zainabu Yusuph kutoka dawati la jinsia na watoto mkoani hapa amesema kuwa ukatili kwa watoto wa kambo au wakufikia hupelekea kuathiri afya ya akili ya mtoto.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mwaka jana ya shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ilionyesha watoto karibu milioni 400 duniani wanakabiliwa na ukatili wa kimwili na kisaikolojia majumbani, kati yao asilimia 60 ni chini ya umri wa miaka mitano.