

7 February 2025, 1:52 pm
Picha ya kamanda wa polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani. Picha na Lilian Vicent
“Wananchi watakiwa kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu”
Na Lilian Vicent
Jeshi la polisi mkoa wa katavi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 118 ambapo kati yao watuhumiwa 37 wamekamatwa wakiwa na mali zinazodhaniwa za wizi.
Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani ambapo watuhumiwa wamejihusisha na wizi wa pikipiki, nondo ambazo ni mali ya maji safi na usafi wa mazingiara [MUWASA ] ,matumizi ya silaha haramu , madawa ya kulevya ,matumizi ya pombe moshi na makosa mengine.
Kwa upande wa kesi za mahakamani jumla ya watuhumiwa 17 wamepatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo mbalimbali katika kesi zinazowakabili.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoani hapa limefanikiwa kuzuia ajali za barabarani kwa kukamata jumla ya makosa 2,231 ambayo yanahususisha ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani.
Jeshi la polisi mkoa wa Katavi limetoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo viovu vya uhalifu pamoja na matukio ya kujichukulia sheria mkononi na kuripoti matukio ya kihalifu.