Mpanda FM

Chatu mwingine aonekana Msasani, hofu yatanda kwa wananchi

4 February 2025, 1:20 pm

Wananchi na viongozi wakisafisha eneo ambalo chatu alimmeza mbwa. Picha na Anna Mhina

“Chatu mwingine aonekana mtaa wa Msasani akimeza mbwa”

Na Anna Mhina

Hofu imetanda kwa wakazi wa mtaa wa Msasani uliopo kata ya Mpanda hotel manispaa ya Mpanda mkoani Katavi kufuatia kuonekana kwa nyoka aina ya chatu katika maeneo hayo akimeza mbwa.

Akizungumza na Mpanda radio FM Ngere Masunga ambaye ndiye mwenye mbwa aliyemezwa na chatu ameeleza namna chatu  huyo alivyomuua mbwa mbele ya macho yake huku wananchi wakieleza namna tukio hilo lilivyowakosesha amani.

Sauti ya wananchi

Kwa upande wao viongozi wa mtaa akiwemo mwenyekiti wa mtaa wa Msasani Juvenary Deus na mwenyekiti wa mtaa wa Kasimba  Benard Nswima wamekiri kuwepo kwa chatu huyo na kuwataka  wananchi  kusitisha shughuli zote katika eneo hilo.

Sauti ya viongozi

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni katika mtaa wa Kasimba jirani na mtaa wa Msasani aliuwawa chatu mwenye urefu wa futi 12 ambaye alikuwa tishio kwa wakazi wa mtaa huo.