

30 January 2025, 12:35 pm
Picha ya mfano wa mtu mwenye msongo wa mawazo.
“Imebainika kuwa chanzo cha watu kujiua ni msongo wa mawazo”
Na Rhoda Elias
Baadhi ya wananchi manispaa ya Mpanda Mkoani katavi wamesema hali duni ya kimaisha na msongo wa mawazo ni miongoni mwa sababu zinasosababisha kukithiri kwa matukio ya watu kujitoa uhai.
Wakizungumza na Mpanda radio FM baadhi ya wananchi wametaja sababu hizo ambapo wananchi wamekuwa wakishindwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo hali inayopelekea kujitoa uhai.
Kwa upande wake mwanasaikolojia Fransisco Wanga ametaja baadhi ya sababu zinazopelekea watu kujitoa uhai huku akiwaasa namna ya kuweza kukabiliana na tatizo hilo.
Wanga ameongeza kuwa endapo mtu alijaribu kufanya jaribio la kujitoa uhai na ikashindikana, mtu huyo anakuwa katika hatari ya kujitoa uhai kwa mara nyingine tena hivyo anapaswa kuchunguzwa mienendo yake.