

27 January 2025, 6:23 pm
Picha ya mwenyekiti wa mtaa wa Kasimba Benard Nswima. Picha na Anna Mhina
“Mtoto wa miaka 7 afariki dunia kwa madai ya kuunguzwa moto”
Na Eda Enock
Mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamisi mwenye umri wa miaka 7 amefariki dunia kwa kifo cha kutatanisha kwa madai ya kuunguzwa na moto mtaa wa Kasimba wilaya ya Mpanda mkoani Katavi .
Mpanda radio imefika sehemu ya tukio ambapo imezungumza na familia ya mtoto huyo na familia imekuwa na mkanganyiko wa kumzika mtoto huyo ambapo upande wa wajomba zake wanadai mtoto afanyiwe uchunguzi huku baba mzazi akidai mtoto huyo azikwe.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Kasimba Bernad Nswima amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Kutokana na madai ya familia mwili wa mtoto huyo umepelekwa hospitali ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ili kuendelea na uchunguzi zaidi.