Mpanda FM

Mwanamke akutwa amejinyonga kijiji cha Magamba

21 January 2025, 4:52 pm

Picha ya Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi. Picha na Anna Milanzi

“Mwanamke mmoja akutwa amefariki dunia kwa kujinyonga na kanga yake”

Na Leah Kamala

Mwanamke mmoja anaesadikiwa kuwa na umri kati ya miaka 19 hadi 22  ambaye jina lake halijafahamika amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga

Taarifa inaeleza kuwa mwili wa marehemu umekutwa ukuning’ing’inia juu ya mti  katika kitongoji cha Makongolo kilichopo  kata ya Magamba manispaa ya Mpanda mkoani katavi .

Akizungumzia tukio hilo  mwenyekiti  wa kijiji  cha  Makongolo Zeno Saidi amebainisha kupokea taarifa kutoka kwa  watoto wanaochunga ng’ombe juu ya uwepo wa mwili wa binti huyo ukiwa umening’inia kwenye mti huku akiwa ana majeraha katika miguu.

Sauti ya mwenyekiti

Kwa upande wao baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa binti huyo ni mgeni katika  eneo hilo ambapo wameiomba serikali iweze kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wasichukue maamuzi yasiyofaa na huku wakilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo ili kupunguza taharuki katika eneo hilo.

Sauti ya mashuhuda wa tukio

Kwa upande wake  kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo majira ya saa 3 asubuhi january 21 2025 na kusema mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na madaktari na  kubaini chanzo cha kifo ni kukosa hewa baada ya kujinyonga.

Sauti ya  Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani

Hata hivyo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya manispaa ya  Mpanda kwa taratibu za mazishi   huku  jeshi la polisi likiendelea kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo.