Mpanda FM

Bodaboda watakiwa kujiunga na mafunzo ya udereva

17 January 2025, 1:05 pm

Sajent Juliana Ibalaja akizungumza na madereva bodaboda wa wilaya ya Mpanda

Dereva bodaboda wanapaswa kuwa na leseni  ili kuondokana na migogoro na askari

Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda wametakiwa  kujiunga na mafunzo ya udereva ili waweze  kutambua sheria za usalama barabarani.

Hayo yamesemwa  na Sajent Juliana Ibalaja  kutoka kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Katavi  katika kikao na madereva bodaboda  kilichofanyika  katika Ofisi za mtendaji wa kata  ya Mpanda Hotel.

 Sajent Juliana amesema  kuwa madereva bodaboda wanapaswa kuwa na leseni  ili kuondokana na migogoro na askari na   kuwataka  kutumia fursa hiyo ili waweze kupata leseni.

Sauti ya Sajent Juliana

Kwa upande wao madereva bodaboda waliohudhuria kikao hicho wameipongeza hatua hiyo na kuahidi kujitokeza kupata  mafunzo ili waweze kujua namna ya kuendesha kwa kufuata sheria za usalama barabarani.

Sauti ya madereva bodaboda

Naye Diwani wa kata hiyo ameahidi kutekeleza mpango wa kuanzishwa kwa mafunzo hayo na kuchangia kiasi cha pesa ili kufanikisha zoezi hilo.

Sauti ya diwani wa kata ya Mpanda hotel