Mpanda FM
Chatu aliyeleta taharuki mtaa wa Kasimba auwawa
17 January 2025, 11:14 am
“Wananchi wameomba msako uendelee kufanyika ili kubaini endapo kuna chatu wengine“
Na Anna Milanzi- Katavi
Wananchi wa mtaa wa Kasimba kata ya Ilembo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameshukuru kwa msako uliofanyika na kufanikiwa kumuua nyoka aina ya chatu huku wakiomba msako uendelee kufanyika ili kubaini endapo kuna chatu wengine.
wametoa ombi hilo baada ya kushuhudia Chatu ambaye ameuwawa ambapo wameomba kuimarishiwa ulinzi ili waishi kwa salama.
Mwenyekiti wa mtaa huo wa Kasimba Benard Nsima ameeleza namna Chatu huo alivyouawa na kuwataka wananchi wa mtaa huo kuchukua tahadhari.
Inaelezwa kuwa chatu huyo aliyeuwawa ana urefu wa futi 12