Katavi:waumini wa kanisa la EAGT kasekese walipokea neno la Krismasi
26 December 2024, 6:12 pm
“kupitia neno la Mungu lililohubiriwa siku ya sikukuu ya Krismasi limeendelea kuwakuza kiimani na kumjua Mungu zaidi“
Na Lilian Vicent-Katavi
Waumini wa kanisa la EAGT lilipo kata ya Kasekese Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wamesema kupitia neno lilohubiriwa na muinjilisti litawasidia kukua kiroho.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio FM mara baada ya kumalizika kwa ibada ya sikukuu ya krismasi.
Sauti za Waumini wa kanisa la EAGT lilipo kata ya Kasekese
Suzana Joshua ambaye ni muinjilishi kutoka Jijini Mbeya wakati akihuribiri katika kanisa hilo amesema kuwa kuzaliwa kwa yesu Kristo ni ukombozi kwa wanadamu.
Sauti ya Suzana Joshua ambaye ni muinjilishi kutoka Jijini Mbeya wakati akihuribiri katika kanisa hilo
Kwa upande wake Peter Majasi Mbalazi mchungaji wa kanisa hilo amewasa wakristo wote kuishi Maisha ya kumtumikia mungu kupitia ibada hiyo ya krismas.
Sauti ya Peter Majasi Mbalazi mchungaji wa kanisa hilo
Ikumbukwe kuwa kila Disemba 25 ya kila mwaka waKristo wote uungana kukumbuka siku ya kuzaliwa kwa bwana yesu Kristo.