Mpanda FM

Wananchi Katavi wasisitizwa kuchagua viongozi bora

20 December 2024, 7:30 pm

Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Mohamed Said Mohamed akiwa na viongozi wengine.picha na Edda Enock

Wapime viongozi kwa vitendo, msiwapime viongozi kwa maneno

Na Edda Enock -Katavi

Wananchi wilayani Nsimbo Mkoani Katavi wametakiwa kuchagua viongozi bora ambao watafanya kazi kwa vitendo na sio kwa maneno ili kutimiza majukumu yao kama viongozi kwa kuzingatia ilani ya chama husika.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Mohamed Said Mohamed ambaye pia ni mlezi wa Chama Mkoa wa Katavi wakati wa hotuba yake akiwa kama mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu huo uliofanyikia viwanja vya shule ya sekondari Nsimbo.

Sauti ya Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Mohamed Said Mohamed

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Idd Kimanta amesema ndani ya mkoa utekelezaji wa ilani ya chama unaendelea hasa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27mwaka huu ambapo asilimia kubwa CCM imechukua ushindi karibu mitaa yote.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Idd Kimanta

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, ameshiriki katika mkutano huo Mkuu ambaye ametoa shukrani zake kwa serikali ambayo inatoa fedha kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye jamii.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Mkutano Mkuu wa utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi CCM ya Mwaka 2020 – 2025 umefanyika mkoani Katavi katika viwanja vya shule ya Sekondari Nsimbo na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa mkoa na wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu katibu Mkuu CCM Zanzibar Mohamed Said Mohamed.