Katavi:Wafanyabiashara wadogo(machinga) wahitaji elimu kuhusu vitambulisho vyao
4 December 2024, 8:16 pm
Wafanyabiashara mkoa wa katavi waomba elimu ya vitambulisho vya wamachinga iendelee kutolewa ili waweze kujua sifa na faida za kitambulisho hicho.
Hayo yamesemwa katika kikao cha pili cha baraza la wafanyabiashara mkoa wa Katavi killichofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa na kusema kuwa kitambulisho hicho kinatakiwa kuwa na ukomo wa kuendelea kukitumia kama machinga.
Sauti ya wafanyabiashara mkoa wa katavi
Kwa upande wake mwenyekiti wa wamachinga mkoa wa Katavi Michael Ernest amesema jitihada za kuwapata wajasiriamali zinafanyika lakini kuna baadhi ya halmashauri wanashindwa kuwatambua wafanyabiashara hao wadogo
Sauti ya mwenyekiti wa wamachinga mkoa wa katavi Michael Ernest
Kupitia kikao hicho ambacho mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ameziagiza halmashauri zote kwenda ktoa elimu ya vitambulisho hivyo kwa kushirikiana na vingozi wa shirikisho la wamachinga mkoa wa Katavi.
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko
Kikao hicho kilijumuisha taasisi mbalimbali za serikali pamoja na wajumbe wa baraza la biashara mkoa wa Katavi na makundi maalumu kama bodaboda na bajaji.