Mpanda FM

Katavi :Wanahabari na wadau wa utamaduni  Wametakiwa  kuibua Urithi wa Utamaduni

12 November 2024, 12:17 pm

Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Katavi ,wadau wa utamaduni pamoja na wakufunzi kutoka TAMCODE.picha na Betord Chove

vijana wanaachana na dhana ya kutegemea ajira serikalini na kujishughulisha na vitu vyao vya asili kujipatia kipato

Na Betord Chove -Katavi

Wanahabari na wadau wa utamaduni  mkoani Katavi Wametakiwa  kuibua Urithi wa Utamaduni usioshikika ili kuvutia wawekezaji  na  kukuza fursa za kiuchumi

Akifunga mafunzo ya Siku mbili , Ofisa utamaduni Manispaa ya Mpanda Bakari Hamza, akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda amewataka wadau wa utamaduni na wanahabari kuyafanyia kazi kwenye jamii.

Sauti ya Ofisa utamaduni Manispaa ya Mpanda Bakari Hamza, akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wanahabari na wadau wa utamaduni wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo waliyopatiwa ili kuhakikisha jamii hususani wanawake na vijana wanaachana na dhana ya kutegemea ajira serikalini na kujishughulisha na vitu vyao vya asili kujipatia kipato

Sauti ya washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wanahabari na wadau wa utamaduni

Mafunzo hayo yameandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (Tamcode) kupitia Mfuko wa UNESCO- Alwaleed Philanthropies.