Katavi :vishikwambi 23 kuongeza ufanisi wa kazi kwa maafisa ugani
8 November 2024, 3:32 pm
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry wa kwanza kulia akikabidhi kishikwambia kwa afisa ugani .picha na John Benjamin
Na John Benjamini-Katavi
Vishikwambi 23 vimegawiwa kwa Maafisa Ugani Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi katika maeneo yao.
Akizungumza wakati wa zoezi la kugawaji vishkwambi hivyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry amewataka Maafisa Ugani hao kuhakikisha wanatumia vitendea kazi hivyo kwa kazi iliyokusudiwa na kuboresha utendaji kazi na kuwasimamia wakulima kwa karibu na kutoa elimu ya upimaji afya ya udongo ili kuongeza uzalishaji na kipato cha mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Sauti ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry wa kwanza kulia akikabidhi kishikwambia kwa afisa ugani .picha na John Benjamin
Kwa upande wake afsa kilimo halmashauri ya Mnaispaa ya Mpanda Gwalusajo Kapande amesema kuwa vifaa hivyo vitakwenda kusaidia kupunguza matumizi ya karatasi huku ikiwa jumla ya wakulima mia saba wamefikiwa kwa ajili ya kupimiwa afya ya udongo.
Sauti ya afsa kilimo halmashauri ya Mnaispaa ya Mpanda Gwalusajo Kapande
Baadhi ya maafisa ugani waliokabidhiwa vishkwambi hivyo wameshukuru serikali kwa kuwapatia vifaa hivyo na vinakwenda kuwasaidia katika majukumu yao ya utumaji wa taarifa za wakulima.
Sauti ya maafisa ugani wakizungumza baada ya kupokea vishikwambi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry wa kwanza kulia akikabidhi kishikwambia kwa afisa ugani .picha na John Benjamin
Serikali nchini Tanzania kupitia wizara ya kilimo imeendelea kuboresha sekta ya Kilimo pamoja na mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi ili waweze kufanya kazi kwa ubora na ufanisi.