Katavi:mtendaji kata apewa adhabu ya kukatwa mshahara kwa kipindi cha miaka 3
8 November 2024, 3:17 pm
kikao cha baraza la madiwani Nsimbo.picha na Rachel Ezekia
“Mtendaji huyo licha ya kuitwa mara kadhaa na mwajiri wake na kuonywa bado aliendelea kutozingatia maagizo ndipo ilipoundwa tume ya uchunguzi kisha kurudisha majibu Hatimaemaamuzi yamefanyika.“
Na Rchel Ezekia -katavi
Baraza la Madiwani katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi, limeazimia kumkata asilimia 15 ya mshahara kwa kipindi cha miaka mitatu Afisa Mtendaji wa Kata ya Katumba kutokana na utovu wa nidhamu ikiwemo kutofika kazini.
Baraza limefanya maamuzi hayo baada ya kujigeuza kuwa Kamati, ambapo limesema Mtendaji huyo licha ya kuitwa mara kadhaa na mwajiri wake na kuonywa bado aliendelea kutozingatia maagizo ndipo ilipoundwa tume ya uchunguzi kisha kurudisha majibu Hatimae leo maamuzi yamefanyika.
Sauti ya Mwenyekiti wa halmashauri ya Nsimbo Halawa Malendeja
Kwa upande wao baadhi ya madiwani waliohudhuria katika baraza hilo wametoa maoni yao juu ya maamuzi hayo yaliyotolewa huku wakitoa wito kwa watendaji kazi wengine kuzingatia miiko na maadili ya kazi ili kukuza mandeleo ya nchi kwa kushirikiana na wananchi
Sauti za baadhi ya madiwani
Mbali na hilo pia baraza hilo limewathibitisha kazini watumishi 73,pia limewabadilishia kada watumishi 18, na kuwapandisha vyeo watumishi 125.