Mpanda FM

Katavi:wananchi watakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya radi wakati wa masika

5 November 2024, 2:46 pm

 Koplo Paul Mtani Masungwa picha na Lilian Vicent

iwapo utakuwa katika njia ya radi ni rahisi kupigwa na radi na kupata madhara

Na Lilian Vicent -Katavi

Kuelekea msimu wa mvua za masika ,wananchi mkoani Katavi wameeleza kuwa moja ya tahadhari ambayo wanaichukua pindi radi inapopiga nikuacha kusimama kwenye miti mirefu ili kujikinga.

Wameyabainisha hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio FM ambapo wamesema ni vyema kuchukua tahadhari kabla ya majanga.

Sauti za wananchi

Afisa habari  Jeshi la zimamoto na ukoaji mkoani Katavi  Koplo Paul Mtani Masungwa amesema iwapo utakuwa katika njia ya radi ni rahisi kupigwa na radi na kupata madhara .

Sauti ya Koplo Paul Mtani Masungwa akitoa elimu dhidi ya radi

Katika hatua nyingine Koplo Masungwa ametoa wito kwa wananchi kutokumshika mtu yeyote iwapo amepigwa radi bila kufahamu mbinu za kufanya maokozi.

Sauti ya Koplo Paul Mtani Masungwa akitoa elimu