Katavi:Takukuru yaokoa fedha zaidi ya Tshs milion 6
1 November 2024, 3:06 pm
kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Stuart Kiondo.picha na Samwel Mbugi
“ametoa rai kwa wananchi wote wa mkoa wa Katavi kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa November 27 mwaka huu“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Katavi imefanikiwa kuokoa fedha kiasi cha shilingi milioni sita laki tisa na tisini Elfu (6,990,000) ambazo zilikuwa zitumike vibaya katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa robo ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Hayo yamesemwa na kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi STUART KIONDO wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari ambapo amesema taasisi imefanikiwa kuokoa kiasi hicho katika robo ya kwanza iliyoanzia julai hadi septemba 2024.
Sauti ya kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Stuart Kiondo
Katika hatua nyingine amesema taasisi ya TAKUKURU imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni mbili laki tano na Hamsini elfu (2,550,000/-) baada ya kubaini uwepo wa matofari 1500 yasio na ubora kwenye mradi wa ujenzi wa mabweni mawili ya shule ya sekondari iliyopo manispaa ya mpanda.
Sauti ya kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Stuart Kiondo
Hata hivyo Kiondo ametoa rai kwa wananchi wote wa mkoa wa Katavi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa November 27 mwaka huu