Mpanda FM

Mwanafunzi apoteza maisha katika bwawa la Milala

6 September 2024, 2:07 pm

Wanafunzi na wananchi ambao wamejitokeza katika mazishi ya mwanafunzi huyo

“waliondoka na walimu wao kurudi kambini walipofikia kwaajili ya kupata chakula ndipo walipogundua mwanafunzi mmoja hayupo”

Na Betold Chove -Katavi

Mwanafunzi aliefahamika kwa majina ya James Japhet (12) amefariki dunia baada ya kuzama kwenye bwawa la maji milala alikopelewa na walimu wake kwa ajili ya masomo kwa vitendo.

Wakizungumza na Waandishi wa habari baadhi ya wanafamilia ya Mtoto huyo wameeleza  namna walivyopata taarifa za msiba wa mtoto wao na namna walivofuatilia ili kujua undani wa tukio hilo kutoka kwa mamlaka husika.

Sauti za wanafamilia wakizungumza

Mashuhuda wa tukio wamesema wanafunzi hao baada ya kumaliza waliondoka na walimu wao kurudi kambini walipofikia kwaajili ya kupata chakula ndipo walipogundua mwanafunzi mmoja hayupo ilibidi warudi kumtafuta katika bwawa walilokuwa wakiogelea.

Sauti ya mashuhuda wakizungumza

Akijibia kuhusu tukio hilo kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi ACP DAVID MUTASYA alioulizwa na waandishi wa habari kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema watakwenda kutolea maelezo kuhusu tukio hilo wakati mwingine.

Sauti ya Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi Katavi

Tukio hilo limetokea katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ambapo mwanafunzi huyo alikua akiogelea na wanafunzi wenzake pamoja na walimu waliowapeleka kwaajili ya masomo kwa vitendo.