Mpanda FM

Wazee mkoani Katavi walia na vilipuzi

3 September 2024, 11:31 am

Baadhi ya wazee wakizungumza na Mpanda radio FM wakitoa malalamiko yao

“Milipuko inayolipuliwa katika uwanja huo imeleta wasiwasi katika jamii na kupelekea baadhi ya wananchi kupata mshtuko wa moyo.”

Na Samwel Mbugi -Katavi

Baadhi ya wazee kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wamemwomba Kamanda wa Jeshi la Polisi Kaster Ngonyani kusitisha mazoezi ya vilipuzi vinavyofanyika katika uwanja wa FFU katikati ya mji.

Hayo yamebainishwa wakati wakizungumza na Mpanda Radio FM kuwa milipuko inayolipuliwa katika uwanja huo imeleta wasiwasi katika jamii na kupelekea baadhi ya wananchi kupata mshtuko wa moyo.

Sauti ya baadhi ya wazee manispaa ya Mpanda wakizungumza

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amesema kuwa amepokea malalamiko hayo na atayafanyia kazi, kwani wapo kwenye mchakato wa kutafuta uwanja wa kufanyia mazoezi sehemu ambayo itakuwa mbali na makazi ya watu.

Sauti ya Kamanda Ngonyani

Ikumbukwe kuwa mwezi wa tano wakati wa uzinduzi wa kusikiliza kero , miongoni mwa kero zilizoibuka ni pamoja na mazoezi hayo yanayofanywa na jeshi la polisi mkoa wa Katavi kwa kutumia vilipuzi.