Tume huru ya uchaguzi yasisitiza ushirikiano Katavi
11 July 2024, 5:10 pm
Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari ambaye ni mjumbe wa tume .picha na Rachel Ezekia
“Tayari halmashauri na majimbo yameshapokea vifaa kwa ajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la mpiga kura”.
Na Rahel Ezekia -Katavi
Tume huru ya uchaguzi imewataka Washiriki wa mafunzo ya maboresho ya daftari la mpiga kura kuzingatia maelekezo yanayotolewa ili kuleta matokeo bora katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Mwezi wa 11 Mwaka huu.
Wito huo umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari ambaye ni mjumbe wa tume katika mafunzo yanayotolewa kwa waratibu uandikishaji mkoa, maafisa uandikishaji , maafisa undikishaji ngazi ya jimbo, maafisa uchaguzi , maafisa ugavi , pamoja na maafisa Tehama wa halmashauri .
Sauti ya jaji wa mahakama kuu Asina Omari ambaye ni mjumbe wa tume
Kwa upande wake Rebeka Msambuse Mratibu wa Uandikishaji wa uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura Mkoa wa Katavi amebainisha kuwa tayari halmashauri na majimbo yameshapokea vifaa kwa ajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la mpiga kura.
Sauti ya mratibu wa uandikishaji wa uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura mkoani Katavi Rebeka Msambuse