Mpanda FM

Sangoma aua wanafamilia Katavi kwa kudai wataacha pombe

9 July 2024, 10:52 am

Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika mazishi .picha na George Rujuba

watu wanatakiwa kuachana na imani za kishirikina kwani matukio kama hayo yanajitokeza kutokana na watu kutomjua Mungu

Na john Mwasomola -Katavi

Watu wawili wa familia moja wamefariki dunia mara baada ya mganga wa kienyeji kuwapatia dawa iliyoelezwa kuwa ni ya kuacha pombe.

Tukio hilo limetokea katika Mtaa wa Kazima Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ambapo Mpanda Radio Fm ilipofika katika mazishi hayo huku Mwenyekiti wa serikali ya mtaa akieleza tukio hilo lilivyokua.

Sauti ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kazima

Kwa upande wake ndugu wa marehemu akizungumzia tukio hilo amesema kuwa jambo hilo limeleta huzuni katika familia, hivyo ameiasa jamii kutoamini imani za kishirikina.

Sauti ya ndugu wa marehemu akizungumzia tukio hilo

Waliofariki dunia ni Paulo Razalo mwenye umri wa miaka 40 na Dismas Razaro mwenye umri wa miaka 44 wote wakiwa ni wakazi wa mtaa wa Kazima Mpanda Mkoani Katavi.