Mpanda FM

Zimamoto Mpanda waaswa kuchukua tahadhari kabla ya kuzima moto

21 May 2024, 3:18 pm

Jeshi la zimamoto lililoundwa kwa sheria namba 14 ya mwaka 2007 jukumu lake kubwa ni kuzima moto na kuokoa maisha na mali katika  majanga yatokanayo na moto ,mafuriko ,teteeko la ardhi ,ajali za barabarani pamoja  na  majanga mengine” Picha na Mtandao

Na Lilian Vicent-Katavi

Wananchi wa mtaa wa Mnazi mmoja kata ya  Uwanja wa ndege  manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamepewa Elimu  kuhusu hatua za kuchukua tukio la moto linapotokea  na vizimia moto vinavyotumika  kulingana na  madaraja ya moto.

Afisa habari wa zimamoto mkoani hapa  Catherine Sambagi   wakati akitoa elimu   amewataka Wananchi kutambua aina mbalimbali za moto ili kupunguza athari zitokanazo na kutumia vizimia moto tofauti kulingana na aina ya moto.

Sauti ya Afisa habari wa zimamoto  Catherine Sambagi   wakati akitoa Elimu

Kwa upande wao baadhi ya Wananchi wa  mtaa huo wamewashukuru jeshi la Zimamoto kwa kufika na kutoa na elimu  kwani itasaidia kupunguza majanga yamoto na wamewakata mamlaka zingine kuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa jamii.

Sauti ya baadhi ya wananchi wa  mtaa wa Mnazi Mmoja wakiwashukuru jeshi la Zimamoto kwa kufika na kutoa na elimu.

Elimu hiyo inayotolewa katika maeneo mbalimbali katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi  ni katika kutekeleza majukumu  ya Jeshi la zimamoto lililoundwa kwa sheria namba 14 ya mwaka 2007 huku jukumu lake kubwa ni kuzima moto na kuokoa maisha na mali katika  majanga yatokanayo na moto ,mafuriko ,tetemeko la ardhi ,ajali za barabarani pamoja  na  majanga mengine.