Mpanda FM

Wafanyakazi mkoani Katavi watoa ya moyoni

1 May 2024, 11:59 pm

Miongoni mwa wafanyakazi waliofika katika viwanja vya Kashaulili kusherehekea maadhimisho ya siku hiyo .picha na Ben Gadau

waajiri wasiopeleka makato katika taasisi zinazopaswa kupeleka fedha hizo wanavunja sheria

Na Ben Gadau -Katavi

Wafanyakazi mkoani Katavi wamelalamikia adha ya waajiri kushindwa kupeleka makato katika mifumo ya huduma za jamii hali inayoshusha weledi wa utendaji kazi

Hayo yamezungumzwa na Avit Anicet Katibu wa Tughe Mkoa wa Katavi wakati akisoma risala katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyoadhimishwa kimkoa katika uwanja wa kashaulili manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

Sauti ya katibu wa Tughe ambaye ni msoma risala akiwakilisha wafanyakazi mkoani humo

Avit Anicet Katibu wa Tughe Mkoa wa Katavi akisoma risala picha na Ben Gadau

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ametoa siku 14 kwa waajiri ambao hawajapeleka michango ya wafanyakazi kupeleka mapema iwezekanavyo.

sauti ya Mkuu wa mkoa wa katavi akizungumza na wafanyakazi hao na kujibu yaliyosomwa katika risala

mkuu wa mkoa wa Katavi alipokuwa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambapo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya kashaulili

Kila ifikapo May 1 kila mwaka dunia huadhimisha siku ya wafanyakazi duniani.