KATAVI, Bidhaa za Vyakula Vilivyoisha Muda Husababisha Kuhara
24 January 2024, 3:43 pm
“Madhara ni kupelekea mtumiaji kupata homa na hata kuharisha kutokana na sumu iliyopo ndani ya Chakula”. Picha Na Mtandao
Na Lilian Vicent-katavi
Baadhi ya wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameeleza maoni yao Mseto juu ya namna wanazingatia muda sahihi wa matumizi ya bidhaa za vyakula kabla Haizijaisha muda wake Wa matumizi.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza Na Mpanda Radio kuwa wanazingatia na wengine wameeleza kwamba hawazingatii Muda wa matumizi sahihi ya bidhaa za vyakula kwakuwa hawaoni madhara yeyote pindi wanapotumia.
Sauti za Wananchi wakieleza kuhusu lewa wa matumizi ya bidhaa za vyakula vilivyyoisha muda wake.
Akizungumza kwa njia ya Simu Mratibu wa Elimu ya Afya kwa uma Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Elizabeth Kakusa amesema moja ya madhara ni kupelekea mtumiaji kupata homa na hata kuharisha kutokana na sumu iliyopo ndani ya Chakula
Sauti ya Mratibu wa Elimu ya Afya kwa uma Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Elizabeth Kakusa.
Katika hatua nyingine amebainisha kuwa wanafanya ukaguzi wa Vyakula sehemu mbalimbali kama vile Madukani, na Viwandani ili kuhakikisha usalama wa bidhaa za Vyakula .