Wananchi Mkoani Katavi wachukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa Wa Kipindupindu
18 January 2024, 12:00 am
Picha na Mtandao
Tahadhari wanazotakiwa kuchukua Wananchi ili kujiepusha na Ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutumia Vyoo bora.
Na Lilian Vicent-Katavi
Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni mseto juu ya tahadhari wanazozichukua kuhakikisha wanajikinga na Ugonjwa wa Kipindupindu.
Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na Mpanda Redio Fm na kubainisha kuwa wanasafisha mazingira yanayowazunguka na kuhakikisha Chakula wanachokitumia ni safi na salama.
Sauti za Wananchi wakieleza uelewa wao na tahadhari wanayochukua dhidi ya Ugonjwa wa kipindupindu
kwa upande wake Afisa afya Manispaa ya Mpanda Eric Kisaka amebainisha kisababishi cha ugonjwa wa Kipindupindu na tahadhari wanazotakiwa kuchukua Wananchi ili kujiepusha na Ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutumia Vyoo bora.
Sauti ya Afisa afya akibainisha sababu za Ugonjwa wa Kipindupindu
Afisa afya Kisaka amewashauri Wananchi kuhakikisha mazingira yanakuwa safi ili kuepuka kusambaa kwa vimelea vya Ugonjwa huo wa Kipindupindu.
Sauti ya Afisa afya akisisitiza Wananchi kufanya usafi