Tanganyika DC yazindua mradi wa urejeshwaji endelevu wa mazingira
17 January 2024, 1:54 pm
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akipanda Mti akikaimu kwa Mkuu wa wilaya ya Tanganyika .Picha na Deus Daudi
lengo la mradi huo ni kuimarisha usimamizi wa pamoja wa mazingira na urejeshwaji wa ardhi iliyoharibiwa ili kujenga uhimilivu wa mfumo wa ikolojia na jamii kwa ujumla
Na Deus Daudi-Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi imezindua Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira kwa kupanda Miti 2,461 katika eneo lililopo katika Kijiji cha Katuma.
Akizungumza baada ya zoezi la upandaji Miti Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf ambaye amekaimu kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika amewataka Wananchi kuutunza na kuuendeleza Mradi huo ili kuleta Matokeo yaliyotarajiwa
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akizungumza baada ya zoezi la upandaji Miti
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila yusuph akitoa hotuba wilayani Tanganyika akimkaimu Mkuu wa wilaya hiyo Onesmo Buswelu. Picha na Deus Daudi
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Dk. Alex Mrema amesema lengo la Mradi huo ni kuimarisha usimamizi wa pamoja wa Mazingira na urejeshwaji wa Ardhi iliyoharibiwa ili kujenga uhimilivu wa mfumo wa ikolojia na jamii kwa ujumla.
Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Dk. Alex Mrema akizungumza
Mradi huo kwa mkoa wa Katavi unatekelezwa katika wilaya ya Tanganyika katika Kata tatu ambazo ni Katuma, Mnyagala na Sibwesa Zinazopakana na Mto Katuma na unatakelezwa kwa kipindi cha Miaka 5 ambapo licha ya upandaji Miti mradi huo unalenga kuhamasisha ufugaji Nyuki kwa kugawa mizinga na upunguzaji wa matumizi ya kuni kwa kugawa Majiko banifu.