Madiwani Halmashauri ya Mpimbwe wajifunza Biashara ya Hewa ukaa
17 January 2024, 12:48 pm
Utunzaji wa Misitu na upandaji Miti unahusisha biashara ya hewa ukaa .Picha na Mtandao
Wanatarajia kuanza kufanya Biashara hiyo kutokana kuwa na Maeneo yanayoruhusu kufanya Biashara ya Hewa ukaa.
Na Betord Benjamini-Katavi
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele Mkoani Katavi wamefanya ziara wilaya ya Tanganyika kujifunza namna Biashara ya Hewa ukaa inavyofanyika.
Wakizungumza baada ya kupata elimu ya Biashara ya Hewa ukaa Mwenyekiti wa halmashauri ya Mpimbwe Silas Ilumba na Mkurugenzi Mtendaji wa halmshahuri ya Mpimbwe Shamimu Mwariko wamesema wanatarajia kuanza kufanya Biashara hiyo kutokana kuwa na Maeneo yanayoruhusu kufanya Biashara ya Hewa ukaa.
Sauti ya Mwenyekiti wa halmashauri ya Mpimbwe na Mkurugenzi Mtendaji wa halmshahuri hiyo wakizungumza
Kwa upande wake Afisa Maliasili wilaya ya Tanganyika Bruno Mwaisaka ameainisha faida zilizopatikana kutokana na Biashara ya Hewa ya ukaa na kusema wanatarajiwa kupata Zaidi ya Bilioni 17.
Sauti ya Afisa Maliasili wilaya ya Tanganyika Bruno Mwaisaka
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya Mlele Majid Mwanga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dk Samia Suluhu Hassan ameshatoa Mwongozo kuhusu Biashara ya Hewa ukaa na kuwataka Watendaji wa Wilaya ya Mlele kuanza utekelelezaji wa Maagizo na kupitia elimu waliyoipata Tanganyika kuanza Biashara ya Hewa ukaa
Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mlele Majid Mwanga akizungumza juu ya elimu waliyoipata