Wazazi Mkoani Katavi Washauriwa Kuzingatia Matumizi Sahihi ya Dawa kwa Watoto
15 January 2024, 10:28 am
Picha na Mtandao
Dawa hizo Mara nyingi huwa zinatolewa kwa Watoto walio na umri chini ya miaka mitano
Na Gladness Richard-Katavi
Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametoa maoni mseto juu ya Matumizi sahihi ya dawa za Maji kwa Watoto wenye umri chini ya Miaka 5.
Wakizungumza na Mpanda Radio Fm Wananchi hao wamesema kuwa kwa kawaida wanatunza dawa na kuzitumia tena pindi Mtoto anapokuwa amepatwa na Maradhi .
Sauti ya wananchi wakieleza juu ya matumizi ya dawa kwa watoto
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Town Clinic Gabriel Elias Amesema kuwa dawa hizo mara nyingi huwa zinatolewa kwa Watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na amewashauri wazazi kuendeleea kufuata ushauri wa mtaalamu wa afya.
Sauti ya Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Town Clinic Gabriel Elias
Elias ameongeza kwa kuwaasa Wazazi kuzingatia Matumizi Sahihi ya dawa kwakuwa kutumia dawa ambazo zimeisha muda wake haziwezi kuwa na msaada kwa Mgonjwa.