Askari wa zimamoto Katavi washauriwa kufanya kazi kwa weledi
20 December 2023, 5:15 pm
Askari wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji Katavi washauriwa kufanya kazi kwa weredi na kuendelea kuwa wavumilivu.
Na Gladness Richard – Katavi
Askari wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji mkoani Katavi wameshauriwa kufanya kazi kwa weredi na kuendelea kuwa wavumilivu pindi wanapokutana na changamoto kazini.
Kuwataka kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu ili waweze kulitumikia taifa kwa utiifu kwa mujibu wa viapo vyao.
Ushauri huo umetolewa na Kamanda mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji kamishina msaidizi Regina Paul Kaombwe Na kuwataka kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu ili waweze kulitumikia taifa kwa utiifu kwa mujibu wa viapo vyao.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Busweru aliyekuwa mgeni Rasmi akimwakilisha mkuu wa mkoa Mwanamvua Mrindoko amempongeza Kamishina Regina kwa utendaji wake mahiri wa kazi ndani na jeshi la zimamoto uokoaji aliyemaliza utumishi wake mkoani Katavi.
Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Katavi Geofrey Mwambungu kwa niaba ya Askari wote wa jeshi hilo amesema kuwa licha ya kuwa ni Kamishina vilevile amesimama kama mama mlezi na kumwomba watakapo pata changamoto katika upande wa kazi asisite kuwaonyesha ushirikiano.