Wananchi Katavi waaswa kukata bima ya afya
20 December 2023, 4:06 pm
Kufuatia uwepo wa sheria ya bima ya afya kwa wote wananchi wa mkoa wa Katavi wametakiwa kukata bima ya afya.
Na Deus Daud – KATAVI
Kufuatia uwepo wa sheria ya bima ya afya kwa wote wananchi wa mkoa wa Katavi wametakiwa kukata bima ya afya ili kusaidia kumudu gharama za matibabu pindi wanapopitia changamoto ya maradhi
Akizungumza na Mpanda Radio Fm Manager wa mfuko wa taifa wa bima ya afya [NHIF] kwa mkoa wa Katavi Ally Endrew Mwakababu amesema kuwa sheria inawataka wananchi wote kuwa na bima ya afya hivyo ni muhimu kwa kujiunga na mfuko wa bima ya afya.
Kwa upande wao wananchi wameeleza namna walivyoipokea sheria mpya ya bima ya afya kwa wote iliyosainiwa hivi karibuni.
Sheria ya bima ya afya kwa wote imesainiwa mwanzoni mwa mwezi Desember na Rais wa Jamuhuri ya Muunganio wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kufuatia uwepo wa mswada wa sheria hiyo toka mwaka 2022.