Ewura yaahidi huduma bora za maji ,umeme, petroli na gesi asilia
18 December 2023, 3:18 pm
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji Ewura imesema inahakikisha mtumiaji anapata huduma bora za maji ,umeme, petroli na gesi asilia.
Na Lilian Vincent – KATAVI
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji Ewura imesema moja ya jukumu lake ni kuhakikisha mtumiaji anapata huduma bora za maji ,umeme, petroli na gesi asilia.
Tobieta Makafu afisa uhusiano muandamizi mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji kanda ya magharibi amesema mamlaka wamekuwa wakihusika kuweka viwango vya bei za maji, masuala ya huduma ya umeme pamoja na kuweka bei za mafuta.
Kwa upande wake muhandisi na Kaimu meneja wa mamlaka hiyo kanda ya maghari walter christopher amesema kwamba moja ya jukumu lao ni kulinda maslahi ya watumiaji
Getrud mbiling’i afisa muandamizi huduma kwa wateja ameongeza kuwa kama mamlaka wana jukumu pia la kutatua migororo ambayo inaweza kutokea baina ya mtumiaji na mhudumu.