Zaidi ya Heka 6 za mahindi zafyekwa na serikali
16 December 2023, 5:23 pm
Kufuatia agizo la manispaa ya Mpanda ambalo linazuia kulima mazao marefu katikati ya makazi ya watu zoezi la kufyeka mazao Kwa ambao walikaidi agizo hilolimeendelea.
Na Mwandishi wetu – Mpanda
Kufuatia agizo la manispaa ya Mpanda ambalo linazuia kulima mazao marefu katikati ya makazi ya watu Wananchi mkoni katavi wamekuwa na maoni tofauti baada ya zoezi la kufyeka mazao Kwa ambao walikaidi agizo hilo.
Wakizungumza na Mpanda Radio Fm wananchi hao wamesema kuwa maamuzi ya kufyeka mazao hayo yamesaidia kuweka mazingira salama na kuweka usawa Kwa wale ambayo hawajalima na pia huku Kwa upande mwingine wakishauri kutoza faini Kwa waliofanya hivyo na si kukata mazao.
Baadhi ya wakulima waliokatiwa mazao wamedai uhalali wa maeneo hayo kwa kuomba vibali katika serikali za mitaa na pia wamekuwa wakilima maeneo kwa muda mrefu huku wakiyawekea ulinzi dhidi ya uhalifu.
Akizungumza kwa njia ya simu kaimu Afisa mazingira manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Geofrey Mbunda amesema kuwa zoezi hilo litakuwa ni endelevu na wale wote ambao wana mazao kwenye maeneo ambayo yalikatazwa yatafyekwa kwa mujibu wa taarifa ya katazo iliyotolewa.
December 13 jeshi la akiba lilipita maeneo ya msasani na Mpanda hotel na kufyeka mazao yote marefu ambayo yapo karibu na makazi ya watu kufuatia agizo linalokataza kulima mazao hayo ambayo yanadhaniwa kuwa sehemu ya kuficha wezi au vitu vilivyo ibiwa.