Mpanda FM

Wananchi watoa maoni mseto kwa wavaa miwani bila kupima

16 December 2023, 12:15 am

Zoezi la upimaji macho. Picha na Mtandao

Wananchi mkoani Katavi watoa maoni juu ya madhara ya kuvaa miwani bila kuzingatia ushauri wa  madktari wa macho.

Na Lilian Vincent – Katavi

Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni juu ya madhara yanayoweza kumpata mtu anaevaa miwani bila kuzingatia ushauri wa  madktari wa macho.

Wakizungumza na Mpanda radio fm   wamesema  moja ya madhara anayoweza kumpata mtumiaji wa miwani bila ushauri wa daktari ni kumpelekea kuwa na uoni hafifu.

Sauti ya Wananchi

Kwa upande wake daktari  kutoka katika hospitali  ya st Aloyce kitengo cha miwani Jeniffer Kessy  amesema kuwa  kuvaa miwani bila kupima kunaweza kumpekea mtumiaji kupoteza uwezo wake wa kuona.

Sauti ya Jennifer Kessy

Aidha Kessy Amewashauri wananchi kuacha kutumia miwani zenye namba bila kuchukuliwa vipimo  na mtaalamu wa macho .