Shule ya Msingi Msasani kunufaika na milioni 14 ya matundu ya vyoo
15 December 2023, 2:40 pm
Serikali yachangia shilingi milioni 14 kwa ajili ya matundu ya vyoo shule ya Msingi Msasani.
Na Gladness Richard – Mpanda
Kufuatia ujenzi unaoendelea Wa shule ya Msingi Msasani Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Serikali imechangia shilingi milioni 14 kwa ajili ya matundu ya vyoo.
Akizungumza na Mpanda Radio FM mwenyekiti wa mtaa wa Msasani amesema wakati ujenzi wa darasa ukiendelea wamepokea kiasi cha fedha Ili madarasa yanavokamilika na matundu ya vyoo yaweze kukamilika.
Kwa upande wao wananchi wa mtaa wa msasani wamesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo kutafungua fursa kwa jamii inayozunguka eneo hilo.
Shule ya Msingi Msasani inajengwa kwa nguvu za wananchi ambapo inavyumba viwili vya madarasa na ofisi moja huku inatarajiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2024.