Jumla ya Miradi 9 inayogharimu zaidi ya Tshs Bilioni Moja inatekelezwa Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi
27 November 2023, 1:37 pm
Kamati ya Siasa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Wakikagua Nyumba ya Watumishi ambayo imekamilika katika Zahanati Kijiji cha Lugonesi Wilaya ya Tanganyika .Picha na Betord Benjamini
Zaidi ya Billion 8 zimepatikana katika Biashara ya hewa ya ukaa kwa Vijiji 8
Na Betord Benjamini -Katavi
Jumla ya Miradi 9 inayogharimu zaidi ya Bilioni Moja inatekelezwa Wilayani Tanganyika kwa kutumia Pesa zilizopatikana kwa Biashara ya Hewa Ukaa.
Akizungumza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi( CCM) Iddy Kimanta Amewataka Wananchi wa Wilaya ya Tanganyika kuendelea kuhifadhi na kutunza Mazingira ili kuendelea kuwapatia Fedha za kutekeleza Miradi na kuwataka Viongozi wa Serikali kuendelea kusimamia Utunzaji wa Mazingira.
Mwenyekiti Ccm Mkoa wa Katavi Iddi Kimanta .Picha na Betord Benjamini
Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Iddy Kimanta
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko Amesema zaidi ya Tshs Billion 8 zimepatikana katika Biashara ya Hewa Ukaa na kunufaisha Vijiji 8 na kuwataka Wananchi kufanya Shughuli za kilimo na Ufugaji katika Maeneo yaliyoelekezwa na kuacha kuingia katika Maeneo yaliyohifadhiwa.
Kamati ya Siasa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa katika Ukaguzi wa Miradi ya Kimaendeleo Wilaya ya Tanganyika.Picha na Betord Benjamini
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa Zahanati Lugonesi, Zahanati ya kijiji cha Lwega,Mradi wa Rea Kijiji cha Lwega, Ujenzi wa Daraja na Ofisi Katika Kijiji cha Lugenesi pamoja na Miradi Mingine ya Afya na Elimu inayopatikana Tarafa ya Mwese.