Tanganyika yanufaika na faida ya mauzo ya tumbaku
24 November 2023, 10:34 am
Uongozi wa Premium Active Tanzania wakikabidhi Mfano wa Hundi yenye Thamani ya Tshs Milion Hamsini na Laki Tatu Kwa Mkuu wa wilaya ya Tanganyika .Picha na Anna Milanzi
Wasimamizi wahakikishe wanakabidhi akaunt za kata hizo kwa kampuni hiyo ili mchakato wa utengenezaji wa madawati ufanyike kwa wakati.
Na Anna Milanzi-Katavi
Kiasi cha Tshs milioni hamsini na laki tatu kimetolewa kwa ajili ya kuchangia huduma za jamii mkoani Katavi huku fedha hizo zikielekezwa katika utengenezaji na usambazaji wa madawati.
Akizungumza katika kikao kilichofanyika wilayani Tanganyika meneja shughuli Nico Roussos kutoka katika kampuni ya Premium Active Tanzania inayojihusisha na ununuzi wa tumbaku kutoka katika vyama vya msingi vya ushirika mkoani Katavi amesema fedha hizo ni sehemu ya faida inayopatikana kutokana na mauzo ya zao hilo.
Sauti ya Meneja Shughuli Kampuni ya Premium Active Tanzania
Meneja Shughuli Kampuni ya Premium Active Tanzania Akisoma Taarifa .Picha na Anna Milanzi
Ameeleza kuwa utaratibu huo unatokana na kiwango cha uzalishaji ambapo pia amezitaja kata nufaika .
Sauti ya Meneja Shughuli Kampuni ya Premium Active Tanzania
Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi amewataka Wasimamizi kuhakikisha wanakabidhi Account za Kata hizo kwa kampuni hiyo ili mchakato wa utengenezaji wa madawati ufanyike kwa wakati.
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akizungumza kwa niaba ya Mkuu Wa Mkoa wa Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu .Picha na Anna Milanzi
Buswelu amewataka Wananchi hasa Wakulima wa Tumbaku kuhakikisha wanapanda Miti ili kufidia Miti inayotumika katika uandaaji wa Tumbaku.
Wadau wa Kilimo cha Tumbaku na viongozi kutoka katika sekta mbalimbali .Picha na Anna Milanzi
Baadhi ya Wakulima wa zao hilo wamesema Kitendo cha Kampuni hiyo Kurudisha Faida kwao kwa kutoa Fedha za kutengeneza madawati kumewapa Nguvu ya kuendelea Kulima zao.
Wakulima wa Zao la Tumbaku wakizungumza