TMA yawataka wananchi kuchukua tahadhari kutokana na mvua.
10 November 2023, 1:44 pm
Mamkala ya hali ya hewa Tanzania TMA imewataka wananchi Katavi kuchukua tahadhari ya kujikinga na madhara ya mvua.
Na John Benjamin – Katavi
Mamkala ya hali ya hewa Tanzania TMA imewataka wananchi mkoani Katavi kuchukua tahadhari ya kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua.
Meneja wa mamlaka ya hali ya hewa mkoa wa Katavi TMA Juma Binda amesema kuwa utabiri wa hali ya hewa kwa msimu huu kwa upande wa mkoa wa Katavi mvua zinatarajiwa kuwa juu ya wastani na wastani ambapo Mvua inatarajiwa kunyesha hadi mwezi 4 mwaka 2024 huku akitoa wito kwa wananchi kufanyia kazi maelekezo ambayo yamekuwa yakitolewa na serikali namna ya kuchukua tahadhari.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi mkoani hapa wameleeza baadhi ya changamoto ambazo wamekuwa wakipitia kama mitalo kujaa maji pamoja na changamoto ya kibiashara.
katika hatua nyingine Binda amewataka wananchi kuhakikisha wanafatilia utabiri wa hali ya hewa wa masaa 24 na siku 5 kwa ajili ya kupata taarifa ya kinachojili kwa upande wa hali ya hewa nchini.