Jamii Katavi yashauriwa kuwa na matumizi sahihi ya uzazi wa mpango
9 October 2023, 2:28 pm
Jamii Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imeshauriwa kuwa na matumizi sahihi ya uzazi wa mpango
Na Kalala Robert & Veronica Mabwile – Mpanda
Jamii Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imeshauriwa kuwa na matumizi sahihi ya uzazi wa mpango ili kuwa na ufanisi mzuri katika njia ya uzazi.
Ushauri huo umetolewa na mratibu wa afya ya uzazi na mtoto manispaa Ya Mpanda wakati akizungumza na kituo hiki na kusema kuwa kutokuwa na matumizi sahihi ya uzazi wa mpango katika jamii husababisha kutakuwa na ufanisi katika njia ya uzazi hivyo ameitaka jamii kufika katika kituo cha afya ili kupata elimu zaidi kuhusiana na uzazi wa mpango na ufanyaji kazi wa uzazi kuwa na ufanisi mzuri.
Wananchi Wakizungumza uelewa kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango wamekubali kuwa ni kweli watu wengi hutumia uzazi wa mpango bila kufika kituo cha afya na kupata elimu mwisho wa siku hupelekea watu kupata mimba zisizo tarajiwa na kupata magonjwa kama kansa ya kizazi.
Sauti ya Wananchi.