Walimu shule za msingi Mpanda wataka ufafanuzi juu ya kupandishwa madaraja
4 October 2023, 2:42 pm
Walimu wa shule za msingi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameutaka uongozi wa mkoa kutolea ufafanuzi malalamiko ya kushindwa kupandishwa madaraja kwa muda mrefu.
Na Ben Gadau – Mpanda
KATAVI
Walimu wa shule za msingi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameutaka uongozi wa mkoa kutolea ufafanuzi juu ya malalamiko ya kushindwa kupandishwa madaraja katika kazi kwa muda mrefu.
Wakizungumza katika kikao kifupi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza mrindoko wamesema kuwa malalamiko ya kushindwa kupandishwa madaraja kwa baadhi ya walimu yameanza tangu mwaka 2019 huku wakiutaka uongozi kumaliza suala hilo.
Benson Ng’amilo katibu msaidizi tume ya watumishi walimu wilaya ya Mpanda amekiri kuwepo kwa malalamiko hayo tangu mwaka 2019 huku akiendelea kuomba serikali kutafuta muarobaini wa kuyamaliza malalamiko hayo.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Katavi mwanamvua hoza mrindoko ameendelea kuwatoa hofu walimu akisema serikali imeyasikia malalamiko hayo na hivi karibuni wataanza kuuona moshi mweupe wa mabadiliko katika kazi zao.